Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Abbas Araghchi, amekutana leo Ijumaa na mwenzake wa Indonesia, Sugiono, katika mji mtakatifu wa Mashhad, ambapo walifanya mazungumzo kuhusu masuala yenye maslahi ya pande mbili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na IRNA, Araghchi alimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia mjini Mashhad, na viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu uhusiano wa Iran na Indonesia pamoja na masuala mengine ya kikanda na kimataifa.
Mkutano huo umefanyika sambamba na ziara ya ujumbe wa ngazi ya juu kutoka Indonesia ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Sugiono, na Spika wa Baraza la Ushauri wa Wananchi, pamoja na wanazuoni na viongozi wa mashirika mbalimbali ya Kiislamu.
Ujumbe huo uliwasili mjini Mashhad kwa lengo la kutoa rambirambi kufuatia kuuawa shahidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Mkuu Sayyid Ali Khamenei (Quds Sirruh), na kuonesha heshima na mshikamano wao na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi hiki cha maombolezo.
Your Comment